BREAKING NEWS.. WORDS FROM PROF JAY AFTER HIS HOUSE TO BE BROKEN Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017. Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. (sijawahi kuumia kiasi hiki 😭) Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. 🤔 Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , LIMENISIKITISHA zaidi. Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo. Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda 🙏🏻. A post shared by Professor Jay (@professorjaytz) on Sep 30, 2017 at 4:07pm PDT Tags : NEWS Facebook Twitter Google+ Pinterest Posted by : Unknown Add Comment Saturday, September 30, 2017 Related Posts :CHECK THIS OUT WHEN TUNDU WAS IN TEST..IT REAL SHOCK (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); … Read More...Costa Rica vs USA – CONCACAF Live Streaming Costa Rica vs USA CONCACAF Gold Cup Semi-final Today 5:00 AM AT&T Stadium, Arlington, … Read More...SUBMISSION OF ARTS AND SCIENCE TEACHERS NAMES (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); … Read More...PUBLIC INFORMATION ON THE THIRD TIMES OF THE TODAY OF 2017 WHERE TO BE REQUIRED TO APPLY IN THE CHETI WARRANTY OR INSTITUTIONS IN THE VIEW OF THE WEEKS OF THE WEEKTIME 2017/2018 The Council wishes to inform graduate six graduates of May, 2017 and the general public; That t… Read More...Real Madrid vs Manchester United Manchester United and Real Madrid are set to go head-to-head in a pre-season friendly at the Lev… Read More...